“Sisi tu Mawakili wa Mungu  tuliokabidhiwa na yeye wakati, fursa, uwezo na mali na mibaraka  ya dunia na rasimali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na wanadamu wenzetu, na kwa kurudisha zaka na kutoa  sadaka kwa ajili yake na kwa utegemezaji na ukuaji wa Kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya  malezi katika upendo na ushindi dhidi yao choyo na tamaa. Wakili hufurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake” (Kanuni ya Kanisa toleo la 17 sura 3-12).

Zaidi ya chochote kingine, kuishi maisha ya kikristo ina maana ya kujitoa – kujisalimisha sisi wenyewe na kumkubali Kristo. Kama vile yeye alivyojitoa kwa ajili yetu, Je sisi tutafanya nini kwa ajili yake?

Mungu hategemei wanadamu kuisukuma kazi yake au kuiendeleza injili. Angeweza kuwatumia malaika kuwa mabalozi wa kweli yake. Angeweza kuwajulisha wanadamu mapenzi yake kama alivyofanya katika mlima wa Sinai kwa sauti yake mwenyewe. Lakini ili kuendeleza roho ya utoaji kujitoa kwetu, amechagua kuwatumia  wanadamu kuifanya kazi yake (Counsels on Steward ship page 20).

Tunapotoa vyote tulivyonavyo kwa Mungu, vyote hivyo humilikiwa na nani hata hivyo? Paulo anasema “Basi mtu yeyote asijisifie wanadamu kwa maana vyote ni vyenu. Kwamba ni Paulo au Apolo au Kefa au dunia au uzima au mauti au vilivyopo sasa au vile  vitakavyokuwepo; vyote ni vyenu; nanyi ni wakristo na Kristo ni wa Mungu.

Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo na Mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu” (1 Kor 3:21- 4:2). Mungu anapovikubali huturudishia kuwa waangalizi, hutufanya kuwa mawakili wa kila kitu tunachomoliki.

Baada ya hapo tabia yetu ya kuishi maisha ya kubweteka, ubinafsi huvunjika kwa kutambua   kwamba Bwana wetu alikuwa uchi, akafungwa na kuwa mgeni. Na agizo lake “Basi enendeni mkawafundishe mataifa yote” hufanya shughuli za Kanisa (Kushirikiana, kufundishana, kuhubiri, kubatiza) kuwa na maana kwetu. Kwa sababu yake  (Yesu) tunapaswa kuwa mawakili waaminifu.

 UWAKILI NINI?

“ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu…………… wala ninyi si mali yenu wenyewe? Maana mlinunuliwa kwa thamani sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu (1 Kor 6:19,20) kwa gharama kubwa tulinunuliwa na kukombolewa. Sisi ni wa Bwana. Hiyo ni kutufanya  kuwa watu wake kwa mara ya pili kwa kuwa alituumba na kutukomboa. Biblia hueleza kwa uwazi kabisa kwamba  Dunia na vyote vilivyomo ni mali yake na wote wakao humo (Zab 24:1)

Ni katika uumbaji Mungu alimshirkisha mwanadamu katika kumiliki na aliendelea kuwa mmiliki wa kweli wa ulimwengu, walezi wakena vitu vyake (Zab 24:1) Ni pale msalabani Yesu alirejesha tena umilikaji baada ya wanadamu kuvitoa vyote kwa shetani. Hivyo sasa amewachagua wanadamu kutumika kama mawakili wa mali zake.

Wakili ni mtu  “aliyekabidhiwa uangalizi wa mali ya mtu mwingine” Uwakili ni nafasi , majukumu. Kwa mkristo uwakili una maana jukumu la mwanadamu kuwa na matumizi ya chochote alichokabidhiwa na Mungu- Uhai, mwili, muda, talanta na uwezo, mali fursa ya kuwahudumia wengine na ujuzi wake wa kweli. Wakristo hutumika kama waangalizi ( Mameneja) wa mali za Mungu na kuangalia maisha kama  fursa ya kimbingu, kujifunza kuwa waaminifu katika uwakili,hutufanya tufae kwa uwakili uliotukuka zaidi na umilele wa maisha ya baadae.

Katika upana wake hivyo basi, uwakili unahusisha matumizi ya busara na kutokuwa  wabinafsi wa maisha.

NAMNA YA KUTAMBUA UWAKILI WA MUNGU.

Maisha yaweza kugawanyika katika sehemu kuu nne za msingi na kila sehemu ni zawadi ya Mungu kwetu.

Mungu ametupatia mwili, uwezo, muda pamoja na umiliki wa mali pamoja na hayo twapaswa kutunza mazingira ya dunia ambayo Mungu ametupatia.

Katika kila taarifa tunavyosoma katika magazeti,taarifa za habari za Luninga (TV) redio, tunaona matukio ambayo ni matokeo ya kupuuzia uangalizi (uwakili) Mungu aliotupatia. Mazingira kuharibiwa, magonjwa na matumizi mabaya ya fedha, umaskini, yote haya ni matokeo ya kupuuzia kanuni za msingi za uwakili katika sehemu zake kuu.

Sehemu ya kwanza- UWAKILI WA MWILI 

Watu wa Mungu ni mawakili wa wao wenyewe twapaswa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote (Luka 10:27).

Wakristo wamepewa fursa ya kukuza nguvu zao za kimwili na kiakili kwa ngazi ya juu. Kwa kufanya hivyo huleta heshima kwa Mungu na kuwakilisha baraka kuu wanadamu wenzao.

Mungu ametuita kama Wakristo kuwa watu wenye afya tele kwani miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu.

Iko mibaraka tele ambayo Mungu ametupatia kuweza kuwa na fya bora. Mibaraka hiyo ni kama ifuatavyo:-

-          Mibaraka ya mazoezi

-          Mibaraka ya mwangaza wa jua

-          Mibaraka ya maji

-          Mibaraka ya Hewa safi

-          Mibaraka ya kuwa na kiasi

-          Mibaraka ya kupumzika.

Uwakili wa mwili ni pamoja na kuuvika mwili mavazi yanayostahili. Wakati ulimwengu unakwenda na mavazi yasiyofaa, wakristo mameitwa kuinua hadhi ya mavazi katika kiwango cha Ukristo.

Sisi tu mali ya Mungu , mwili nafsi na Roho kwa hiyo  ni wajibu wetu wa kidini kushika sheria za afya, kwa ajili ya vyote, hali njema na furaha yetu sisi wenyewe, na pia  kwa ajili ya huduma yenye ufanisi kwa Mungu na  kwa wanadamu wenzetu. Hamu ya kula chakula sharti idhibitiwe. Afya hutumiwa kwa kuzingatia  akili kwa kanuni za afya zinazohusiana na hewa safi, upitishaji wa hewa safi,nguo zifaazo,usafi,mazoezi ya kufaa na maburudisho,usingizi tosha  na pumziko na lishe tosha  iletayo siha. Mungu amempa mwanadamu chakula chema cha aina nyingi ili kutosheleza kila hitaji la lishe; matunda, nafaka, njugu na mboga zilizoandaliwa kwa njia rahisi pamoja na maziwa………………. hufanya lishe yenye afya mno” (Christian Temperancy  and Bible Hygene Uk 47).

 Wakristo waepuke kuonyesha  urembo na madoido mengi  ikiwezekana nguo ziwe za namna bora na rangi zinazopendeza na zifaazo kwa huduma. Zichaguliwe kutokana na kudumu kwake  kuliko kwa ajili ya onyesho.Uvaaji udhihirishe na adabu nzuri heshima na zinazofaa kwa onyofu wa asili (Messages to Young people Uk 352).

 Neno la Bwana linabakia pale pale, likisema “ Ninyi ni nuru ya Ulimwengu mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango, nayo yawaangaza wote walioko nyumbani. Vivyo hivyo Nuru yenu na iangaze mbele ya watu wapate  kuyaona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni” (Matayo 5: 14:16)

Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri, kujisikia na  kutenda kulingana na kanuni za mbinguni. Ili Roho aumbe  upya ndani yetu tabia ya Bwana wetu twapaswa kujihusisha tu katika  mambo yale ambayo yatazaa katika maisha yetu usafi unaofanana na Kristo, hii italeta afya na furaha katika maisha yetu. Hii inamaanisha kwamba maraha na maburudisho yetu yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji na uzuri wa Kikristo. Huku tukitambua  tofauti za Kiutamaduni, mawazo yetu yanapaswa yawe ya kawaida si ya anasa na safi yanayostahili wale ambao uzuri wao wa kweli asili yake sio mambo ya nje bali asili yake ni mapambo yasiyoharibika yenye  Roho ya upole na utulivu. Pia inamaanisha kwamba   kwa kuwa miili yetu ni mahekalu ya Roho mtakatifu yatunapasa kutumia kwa akili. Pamoja na  mazoezi tosha na mapumziko, yatupasa kuchagua lishe  yenye afya. Kwavyovyote vile  twapaswa kuepuka  vyakula  vilivyo najisi vilivyotajwa kwenye maandiko matakatifu. Kwa vile madawa hudhuru miili yetu, yatupasa kuepukana navyo pia. Badala yake tunapaswa  kujishughulisha na chochote kile kinacholeta  mawazoni mwetu na miili yetu  nidhamu ya Kristo ambaye hutamani uzima wetu , furaha na wema.

Mafungu ya ziada

Warumi 12:1, 2.  1Yoh 2:6, Waef 5:1-2; Waf 4:8 2 Kor 10:5, 6 14-7, 1 Pet 3:1-4; 1 Wakr 6: 19,20 10:31; Walawi 11: 1-4, 7, 3 Yoh 2

SEHEMU YA PILI-WAKILI WA TALANTA

Kila mmoja wa watoto wa Bwana amepewa uwezo; mmoja aweza kupewa uwezo wa uimbaji, mwingine uwezo wa Biashara au ufundi wa magari au mmoja aweza kutengeneza marafiki kwa urahisi lakini mwingine hutenda kazi kwa ukimya lakini kutenda kazi kwa umakini na kwa uzuri wote.

Kila uwezo waweza kutumika kumtukuza mwenye kutumia au kumtukuza yeye aliyeitoa ambaye ni Mungu wa mbinguni.

Maneno ya Yesu mwenyewe aliyoyasema kabla  hajapaa kwenda Mbinguni alisema “Enendeni Ulimwenguni mwote” aliwaagiza wanafunzi wake kuhubiri injili kwa kila kiumbe. Mungu anapotoa kazi hutoa pia vitendea kazi, alipowaagiza kuwa watu waende aliwapa uwezo.

Kusudi la vipawa vya Roho kwa Wakristo ni kuwawezesha kutimiza utume wa kanisa pamoja na ukuaji wake.

 Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia  katika huduma ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya kanisa na wanadamu zikitolewa kwa wakala wa Roho mtakatifu, ambaye humgawia kila mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa na kanisa katika kutekeleza shughuli zake zilizoamuriwa na Mungu kulingana na maandiko, karama hizi hujumuisha huduma kama imani, uponyaji, unabii, mahubiri, mafundisho na ufadhili kwa ajili ya msaada na faraja kwa watu.

Baadhi ya washiriki hitwa na Mungu na kukirimiwa  na Roho kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji,uinjilisti, utume na huduma za kufundisha zinazohitajika hasa  kuwapatia  zana washiriki kwa ajili ya huduma, kulijenga kanisa  hadi ukomavu wa Kiroho na kukuza umoja wa imani na maarifa ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama mawakili waaaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, Kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu ya mafundisho ya uongo na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa Mungu na kujengeka imara katika Imani na Upendo (Warumi 12:4-8; Wakor 12:9-11, 27, 28 Waef 4:8, 11:1-6; Mdo 6:1-7; Tim 3:1-13; 1 Pet 4:10,11).

 

SEHEMU YA TATU-WAKILI WA WAKATI (MUDA)

Mungu ametupatia  wakati. Muda wapaswa kutumika  kwa angalifu. Biblia inasema “Lolote mfanyalo, lifanyeni  kwa moyo, kama kwa Bwana wala si kwa wanadamu mkijua ya kuwa kwa Bwana kuna  ujira wa urithi” (Kol 3,23,24).

Neno la Bwana linatuambia tusiwe wajinga tuwe werevu,tukiukomboa wakati kwa sababu zamani hizi ni za uovu. (Waefeso 5: 15, 16) Kama Yesu twapaswa kuwa kwenye shughuli za Bwana (Luka 2:49).

 

Muda ni zawadi kutoka kwa Mungu. Muda umetolewa kutengeneza tabia kwa ajili ya ufalme wa Mbinguni.

 

Voltaine siku moja alisema kuwa kuna njia ne za kupoteza muda:-

-          Kutofanya chochote

-          Kutofanya kile ulichopaswa kufanya

-          Kufanya vitu kwa uzembe

-          Kutofanya vitu kwa wakati.

Ili kuonekana mawakili waaminifu Wakristo wanapswa kujiondoa wenyewe katika hali za namna hiyo.

Mifano ya wakati

-          Kwa Wayunani – Muda ni mstari una mwanzo una mwisho.

-          Kwa Wayahudi na watu wa Asia – Muda ni duara

-          Kwa Waislamu – Mungu ameunda kila kitu , haina maana kwa mtu kufanya chochote.

-          Africa – Muda hauna maisha ya baadae (future) mtu huishi kwa yaliyopita- maisha ya baadae hayapo sana kwenye lugha za Kiafrika.

-          Mabudha – Muda ni mzunguko unaojirudia wenyewe

-          Hata kwa wazungu muda una mtazamo.

Wafaransa wanasema – Nina miaka 30 wakiangalia muda.

Waingereza wanasema – Nina miaka 30 wakiangalia umri.

Waamerika  husema – Muda ni pesa.

Mtazamo wako ni nini?

 

Wakati ndani ya Biblia Marko 1:15,

-          Zawadi ya Mungu kwa wanadamu

-          Mungu hufanya kazi kwa wakati

-          Kristo mhimili wa wakati

-          Mtu hapaswi kufanya lolote atakalo bali apaswa kufanya pale Bwana anapomuagiza.

Mungu ndie mtoaji wa muda Zab: 10: 12 “ Utufundishe kuzihesabu siku zetu

Mungu yuko makini na muda Zab: 31: 16 muda wangu u mkononi mwako, Daniel 2:21 Yeye ndie anayeweza kubadili nyakati.

Kila jambo na wakati wake. Muhub 3:1, 8:6  Kuna wakati katika  kila jambo.

SEHEMU YA NNE-UWAKILI WA MALI

Mungu aliwapatia wazazi wetu wa kwanza  jukumu la kuitawala Dunia kutawala  wanyama kwa aina zake pia kutunza Bustani ya Eden (Mwan 1:28; 2:15) Hii  yote ilikuwa sio kufurahia bali pia  kuangalia (Manage), jambo moja  lilikuwa kama sharti kwao lilikuwa  kutokula mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mti huu ulikuwa kwa ajili ya kuwa kumbusha kuwa Mungu mmiliki na wenye mamlaka ya mwisho Duniani hapa. Kwa kutunzasharti hili wawili hawa walionyesha  imani yao na utii wao kwao.

Baada ya kuanguka Mungu hakuweka kipimo cha  utii katika mti. Lakini bado wanadamu walihitaji kukumbushwa kuwa  Mungu ni chanzo  cha vitu vyote vyema (Yakobo 1: 17) na kuwa yeye ametupatia nguvu kupata tulivyo navyo. (Kumbku 8:18) Ili kutukumbusha  kuwa yeye ni chanzo cha kila  mmbaraka, Mungu alianzisha mfumo wa zaka na sadaka.

Mfano huu wa zaka na sadaka  uliokuwa namna ya  kutegemeza ukuhani kipindi cha waisrael. Wakristo  leo wameuchukua kama mfumo wa  kibiblia katika  kuisaidia kazi ya injili Duniani kote. Mungu ameubariki mfumo wa  kushirikiana  habari njema kwa kuchangia  zaka na sadaka za watu wake.

Zaka – kama vile moja ya saba ya muda wetu  tunavyouweka kwa Bwana, vivyo moja ya kumi ya mali zetu twaziweka kwa Bwana pia. Biblia inatuambia zaka ni “Takatifu kwa Bwana”  ikiashiria  kuwa yeye ni  mmiliki wa kila kitu. (Kumb 27:30,32)

Mungu anapoitisha zaka (Mal 3:10) hafanyi hivyo kama shukrani au ukarimu. Ingawa shukurani yapaswa kuwa sehemu ya kumwonyesha Mungu.  Tunatoa zaka  kwa kuwa Mungu ameamuru hivyo. Zaka ni ya Bwana  na ameagiza  tumrudishie.

-          Mifano ya utoaji wa zaka

Mwan 14:20 – Abraham alitoa zaka wa Melkzedeki 

Mwab 28:22 – Yakobo  pia alitoa zaka.

Kumb 27:30 – 32

Heb    18:24,26,28           Israel wanaagizwa  kutoa zaka.

Nyakati 12:6,11,17

Sadaka  - Wakristo wenye shukurani hawawekewi  mipaka katika  michango  yao kanisani. Katika  Israel hekalu lilijengwa kwa sadaka za  hiari ya  moyo (kut 36:2 -7), Nyakati 29:14). Sadaka maalumu zilisaidia kufanya matengenezo katka sehemu za Ibada (Kuto 30:12 – 16) 2 Falme 12:4,5; Kumb 24:4 -13; Nehe 10:32,33).

 Leo pia Mungu anatuita kutoa  kwa kadri tulivyobarikiwa.  Sadaka zahitajiwa kujenga na kukarabati makanisa. Hii ikiwa ni pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali za kanisa katika kutimiza utume.

SEHEMU YA TANO-UWAKILI WA KUTUNZA DUNIA.

 Katika  miaka ya hivi karibuni wanasayansi na wana mazingira wamegundua kuwa Dunia  inaharibiwa na hivyo kama matokeo ya uharibifu huu Dunia itakuwa sio mahali  pa kuishi.

 Katika hili tumeitwa kuwa mawakili wa dunia hii . Twapaswa kutumia kila njia  kuhakisha tunaitunza dunia kama tulivyoagizwa (Mwan 1:26) Yesu anapokuja mara ya pili kristo  atawaharibu wale wanaoharibu Dunhia (Ufunuo 11:18) kwa mtazamo  huu mawakili wa kikristo  wanahusika sio katika mali walizopewa pekeyake hata katika ulimwengu  unaowazunguka.

MIBARAKA YA UWAKILI.

Mungu ametupatia jukumu la uwakili kwa ajili ya manufaa yetu na wala sio kwa manufaa yake.

- Mibaraka binafsi.

Sababu mojawapo ambayo Bwana anaendelea kutuambia  kuweka maisha yetu yote, uwezo, mwili na mali,  hivyo ni kuendeleza maisha yetu ya kiroho, tunapo  yafanya haya yote tunapalilia upendo  ambao Mungu  ameupandikiza ndani yetu.

- Uwakili hutusaidia  kuondoa tabia za uchoyo ambazo Yesu amezikemea. (Luke 12:15).

Kwa habari ya zaka na sadaka Bwana ameahaidi baraka tele hata isiwemo nafasi ya  kutosha au la, Biblia inasema   “……………mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.